Dataset Viewer
Auto-converted to Parquet Duplicate
name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesisitiza umuhimu wa kufanyika mambo matano kuelekea uchaguzi
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesisitiza umuhimu wa kufanyika mambo matano kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, akiyataja kuwa nyenzo ya kuongeza ushiriki wa wananchi na imani yao kwa uchaguzi huo. Miongoni mwa mambo hayo ni wananchi kuhakikishiwa dosari zilizotokea mwaka 2019 hazitokei tena, kupewa uhuru wa...
Mwanahabari wa kujitegemea, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lil
Mwanahabari wa kujitegemea, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lililozuia kuendelea kwa kesi yake anayokabiliana na Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania Ltd. Kabendera aliifungua kesi hiyo, Julai mwaka huu, akiituhumu kampuni hiyo kuhusika na utoaji wa taarifa za mahali alip...
Kama mara yako ya mwisho kufika Dar es Salaam ni miaka 10 iliyopita, pengine unahitaji mwenyeji wa k
Kama mara yako ya mwisho kufika Dar es Salaam ni miaka 10 iliyopita, pengine unahitaji mwenyeji wa kukupokea na kukuelekeza maeneo mbalimbali ya jiji hili. Hilo linatokana na ukweli kwamba, karibu kila kitu kimebadilika kuanzia barabara, majengo marefu kwa mafupi na hata kuwapo kwa miji mipya kumeibadili Dar es Salaam...
Kama uliwahi kujiuliza ni lini Tanzania itatekeleza miradi yake kwa makandarasi wake wa ndani, huu n
Kama uliwahi kujiuliza ni lini Tanzania itatekeleza miradi yake kwa makandarasi wake wa ndani, huu ni wakati sahihi na jawabu la swali hilo kupatikana. Sababu ya maswali kama hayo ni uhalisia wa mwenendo wa utekelezwaji wa miradi mbalimbali nchini, ambayo aghalabu walipewa makandarasi kutoka nje ya nchi. Kilichosabab...
Moja ya alama kuu za juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi, ni ujenzi wa
Moja ya alama kuu za juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi, ni ujenzi wa Daraja la JP Magufuli, ambalo awali liliitwa Kigongo Busisi. Mabadiliko ya jina la daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 yana uhusiano wa moja kwa moja na historia ya Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. Jo...
Licha ya uwepo wa vivuko vya watembea kwa miguu kutazamwa kama muarobaini wa ajali barabarani, kwa b
Licha ya uwepo wa vivuko vya watembea kwa miguu kutazamwa kama muarobaini wa ajali barabarani, kwa baadhi ya wananchi vimekuwa kama vikwazo. Hatua ya kuviona vikwazo inatokana na kile kinachoelezwa na baadhi yao kuwa, urefu wake, uvivu wa kupanda unawalazimu wakatize barabara badala ya kutumia vivuko hivyo. Hata hivy...
Ni saa 144 zinazounda siku sita, ndio jumla ya muda ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameutumia mkoani
Ni saa 144 zinazounda siku sita, ndio jumla ya muda ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameutumia mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi. Kwa mtazamo wa wanazuoni, ziara hiyo kwa maneno machache inatafsiriwa kuwa ya maelekezo, utatuzi kero, fursa na matumaini kwa wakulima. Mtazamo huo wa wanazuoni, unaakisi uhalisia wa mlolong...
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaoacha taarifa za uzus
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaoacha taarifa za uzushi zisambae bila kuzikanusha. Kinachomkera zaidi ni kile alichofafanua, pamoja na uzushi huo aghalabu hutokea na kuyahusu maeneo yenye wawakilishi wa Serikali, lakini wanasubiri viongozi wa kitaifa waje kukanusha. Kaul...
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sambamba na Serikali kuanza ujenzi wa bandari ya Mbambabay, pia ina
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sambamba na Serikali kuanza ujenzi wa bandari ya Mbambabay, pia inatarajia kuzungumza na Serikali ya Malawi juu ya ushirikiano katika huduma za bandari hiyo. Hatua hiyo kwa mujibu wa Rais Samia, inalenga kufungua milango ya ushirikiano wa kibiashara kupitia bandari hiyo kwa mataifa hay...
Kama ulidhani kuzaliwa kwako na baba na mama kunakupa uhalali usio na shaka wa kurithi mali walizona
Kama ulidhani kuzaliwa kwako na baba na mama kunakupa uhalali usio na shaka wa kurithi mali walizonazo unakosea, lipo takwa la kisheria linalokuondolea haki hiyo, ingawa mwenye mali ni baba au mama yako wa damu. Pengine huu unaweza kuwa ukweli mchungu kwa baadhi ya warithi, kutokana na uhalisia wa matukio kadhaa ya ug...
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imebadili mfum
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imebadili mfumo wa utendaji wake, ikitangaza kubadili mfumo wa utekelezaji wa majukumu yake, kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia ubia (PPP). Kutokana na mabadiliko hayo, Temesa imewaita wawekezaji wa sekta binafsi kutoka ndani ...
Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na gharama za uzalishaji wa
Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na gharama za uzalishaji wa kilimo, matumizi ya nishati ya umeme jua hasa kwenye umwagiliaji yanatazamwa kama suluhisho. Teknolojia hiyo sio tu inapunguza gharama za kilimo, bali inachangia kuongeza uzalishaji wa mazao, hasa katika maeneo yenye uk...
Rais Samia Suluhu Hassan ameyajibu matamko ya balozi zinazoyawakilisha mataifa mbalimbali nchini, ya
Rais Samia Suluhu Hassan ameyajibu matamko ya balozi zinazoyawakilisha mataifa mbalimbali nchini, yaliyotaka uchunguzi wa haraka wa matukio ya utekaji na mauaji ya watu, akisema Tanzania ni nchi huru haipaswi kuelekezwa cha kufanya kwenye mambo yake. Katika majibu yake hayo, amewashutumu mabalozi hao akisema walichoki...
Tofauti na ilivyo katika maeneo mengi, kila jina la mtaa unaounda Kata ya Kimara ni simulizi yenye h
Tofauti na ilivyo katika maeneo mengi, kila jina la mtaa unaounda Kata ya Kimara ni simulizi yenye historia maridhawa. Uwepo wa viwanda, shughuli za kiuchumi na miradi mbalimbali, ndiyo msingi wa ubatizo wa majina hayo, yanayoendelea kutumika hadi sasa. Unapotokea mjini kati Dar es Salaam, Mtaa wa Kibo ndilo lango la...
Licha ya mtazamo kuwa, kuimarika kwa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) kutaathiri usafiri wa anga kwa
Licha ya mtazamo kuwa, kuimarika kwa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) kutaathiri usafiri wa anga kwa upande mmoja, wadau wa usafiri huo, wamesema reli hiyo ya kisasa inaweza kuimarisha sekta ya anga pia. Matumaini ya wadau hao yanatokana na mtazamo kuwa, kuna uwezekano wa vyanzo hivyo vya usafiri kushirikiana na kuwapa...
Wakati Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na wadau wengine wakisisitiza uchunguzi huru dhidi ya m
Wakati Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na wadau wengine wakisisitiza uchunguzi huru dhidi ya matukio ya utekaji na mauaji, Serikali imesema kwanza jamii inapaswa kujiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila unapokaribia uchaguzi. Katika hoja yake hiyo, Serikali imesema ni rahisi kutupa lawama kwa Jeshi la Polis...
Hisia na mitazamo tofauti imeibuka juu ya sheria inayomtaka mama kuacha wazi eneo linalopaswa kuandi
Hisia na mitazamo tofauti imeibuka juu ya sheria inayomtaka mama kuacha wazi eneo linalopaswa kuandikwa jina la baba wa mtoto katika cheti cha kuzaliwa, iwapo mzazi huyo wa kiume hajulikani au kuna sababu za kutoandikwa. Mitazamo hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi Digital iliporipoti kuhusu takwa la mama ...
Kutokana na kuongezeka kwa mwamko wa abiria kutumia usafiri wa treni ya umeme (SGR), wamiliki wa mab
Kutokana na kuongezeka kwa mwamko wa abiria kutumia usafiri wa treni ya umeme (SGR), wamiliki wa mabasi nchini wamekuja na mikakati mipya kuhakikisha wanaendelea kuwa sokoni bila biashara zao kuathirika. Tangu kuanza kwa usafiri huo, wamiliki wa mabasi wamekuwa wakilalamikia changamoto katika soko na tayari wengine wa...
Licha ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku maandamano ya Chadema, chama hicho kimesema kitu pekee kita
Licha ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku maandamano ya Chadema, chama hicho kimesema kitu pekee kitakachositisha mpango huo ni jeshi hilo kuwarejesha viongozi wote waliotekwa wakiwa hai au wafu. Mpango wa maandamano ulitangazwa Septemba 12 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kushinikiza kurudishwa kwa viongozi wak...
Usisubiri hadi kumbukumbu yake ya kuzaliwa au kumbukizi ya siku ya ndoa ‘anniversary’ kumwonyesha mk
Usisubiri hadi kumbukumbu yake ya kuzaliwa au kumbukizi ya siku ya ndoa ‘anniversary’ kumwonyesha mkeo thamani yake maisha mwako, unajua ipo siku rasmi ya kuadhimisha kumuenzi mke. Kwa lugha ya kimombo inaitwa ‘Wife Appreciation Day’. Siku hiyo inayoadhimishwa Septemba 15 (leo), kila mwaka imeteuliwa kuwa maalumu kwa ...
Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha demokrasia katika kipindi ambacho, wanazuoni na ri
Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha demokrasia katika kipindi ambacho, wanazuoni na ripoti mbalimbali zinaonyesha dosari katika misingi ya demokrasia ya nchi. Kwa mitazamo ya wanazuoni hao, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ndiyo uliokuwa ukomo wa safari njema ya demokrasia nchini, baada ya kushuhudiwa mising...
Baadhi ya wanazuoni na wadau wa haki jinai, wamesema hatua ya kuibua tuhuma zinazolichafua Jeshi la
Baadhi ya wanazuoni na wadau wa haki jinai, wamesema hatua ya kuibua tuhuma zinazolichafua Jeshi la Polisi, inawatengenezea sumu wananchi na hivyo wanajenga dharau kwa chombo hicho cha ulinzi na usalama. Dharau hizo kwa mujibu wa wadau hao, matokeo yake ni vitendo vya uvamizi wa vituo vya polisi na hatimaye kulifanya ...
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNF), Joseph Butiku amewataka viongozi wa vyombo vy
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNF), Joseph Butiku amewataka viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wasiseme hawawajui wahusika wa uhalifu, kufanya hivyo kunaondoa sababu za wao kuwa na nafasi walizonazo. Ameisisitiza hoja yake hiyo kwa kuweka wazi kuwa, wahalifu wa utekaji, mauaji na ulawiti wanaj...
Mataifa mbalimbali duniani yameeleza kusikitishwa na taarifa za vitendo vya ukatili, kupotea na vifo
Mataifa mbalimbali duniani yameeleza kusikitishwa na taarifa za vitendo vya ukatili, kupotea na vifo dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu na kisiasa nchini, huku yakisisitiza uchunguzi wa haraka kubaini wanaohusika. Masikitizo ya mataifa hayo 15 yanayounda Umoja wa Ulaya (EU) yalitolewa na balozi zao zilizopo nch...
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza mamlaka za uchunguzi zichunguze matukio ya mauaji, wadau
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza mamlaka za uchunguzi zichunguze matukio ya mauaji, wadau wamependekeza njia mbadala ya uchunguzi huo, wakitaka vyombo vya dola visihusike kutekeleza jukumu hilo. Kwa mujibu wa wadau hao, kamisheni maalumu inapaswa kuundwa na mkuu huyo wa nchi itakayohusisha vyombo mbalimbali...
Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili nyeupe zilizoandikwa kwenye vibao vyeusi, ndizo zilizotajw
Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili nyeupe zilizoandikwa kwenye vibao vyeusi, ndizo zilizotajwa na mashuhuda kuhusika katika tukio la ukamatwaji wa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao Septemba 6, mwaka huu. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, tukio hilo lilitokea saa 1 jioni, muda ambao tayari giza lilishaanz...
Saa chache baada ya kuripotiwa kwa mauaji ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Ally Kibao, Jeshi la
Saa chache baada ya kuripotiwa kwa mauaji ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Ally Kibao, Jeshi la Polisi limesema limeanza uchunguzi mkali kubaini wahusika wa mauaji hayo ili wachukuliwe hatua za kisheria. Taarifa za kuuawa kwa Kibao zilisambaa leo, Septemba 8, 2024 katika mitandao ya kijamii, baada ya mwili wake ku...
‘Ni utata mtupu’ ndiyo maneno yanayoakisi tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, All
‘Ni utata mtupu’ ndiyo maneno yanayoakisi tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao lililotokea siku moja baada ya kukamatwa akiwa katika usafiri wa umma kwenda nyumbani kwao mkoni Tanga. Kinachojenga msingi wa utata ni mazingira ya kukamatwa kwake kulikofanyika Tegeta, mbele ya Jengo la Kibo C...
Wimbi la vitendo vya mauaji katika siku za hivi karibuni, limehusishwa na kukithiri kwa matatizo ya
Wimbi la vitendo vya mauaji katika siku za hivi karibuni, limehusishwa na kukithiri kwa matatizo ya afya ya akili, kumomonyoka kwa maadili, uelewa duni wa namna ya kuishi, huku umasikini uliopitiliza nao ukitajwa kama moja ya sababu. Kwa mtazamo wa kisaikolojia, wanazuoni wanasema vitendo hivyo ni dalili ya jamii kupu...
End of preview. Expand in Data Studio
README.md exists but content is empty.
Downloads last month
15